Mali imejikatia tikiti ya kushiriki fainali ya mchuano wa kuwania ubingwa wa Afrika miongoni mwa wachezaji wanaoshiriki ligi za nyumbani CHAN dhidi ya Congo DR baada ya kuilaza Ivory Coast 1-0 katika nusu fainali ya pili iliyochezwa katika uwanja wa taifa wa Rwanda.
Mali ambayo ilikuwa imefuzu kwa nusu fainali yake ya kwanza ya CHAN ilipata bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika mbili tu mechi hiyo ikamilike.
Bao hilo lilitiwa kimiani na YVES BISSOUMA kunako dakika ya 88'ya kipindi cha pili.
Sinayoko alimmegea pasi safi Bissouma naye hakusita alipiga chenga moja na kumbwaga kipa wa The Elephants Badra .
ALI BADRA alikuwa ameiokoa Ivory Coast mapema alipopangua mkwaju wa Coulibaly katika dakika ya 33'' ya kipindi cha kwanza.
Timu hiyo sasa imejikatia tikiti ya kuchuana dhidi ya Congo DRC katika fainali siku ya jumapili.
Leopards ya Congo DR ambaye ilitamausha Guinea mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti hapo jana.
Guinea kwa upande wake sasa itachuana dhidi ya Ivory Coast kuamua mshindi wa tatu.
Fainali itaandaliwa siku ya jumapili.
Miongoni mwa wale walioshuhudia mechi hii ya kukata na shoka ni wagombea wa kiti cha urais wa FIFA Tokyo Sexwale, Gianni Infantino na Jerome Champagne.
Watatu hao waliketi pamoja katika uwanja huo wa Stade de Kigali .
Kuwepo kwao huko Rwanda kumetokana na habari za kuaminika kuwa shirikisho la soka barani AfriKa linaandaa mkutano wa wenyeviti wa mashirikisho ya kandanda ya mataifa wanachama.
Mkutano huo wa Ijumaa usiku unapangiwa kutoa mwelekeo wa ni mgombea yupi watakayemuunga mkono katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari tarehe 26.
Mali imejikatia tikiti ya kushiriki fainali ya mchuano wa kuwania ubingwa wa Afrika miongoni mwa wachezaji wa nyumbani dhidi ya Congo DR baada ya kuilaza Ivory Coast 1-0.
0 maoni:
Chapisha Maoni