Nyota wa muziki wa
Hip Hop nchini Marekani DMX ametoka hospitalini baada ya kushindwa
kupumua na kulazimika kusaidiwa kufanya hivyo katika eneo la kuegesha
magari ndani ya hoteli moja mjini New York.
Wakili wa nyota huyo
wa Rap, Murray Richman amethibitisha kwamba amepona baada ya kuanguka
katika mji wa Yonkers siku ya jumatatu.Bwana Murray amesema kuwa hakujua kilichosababisha msanii huyo kushindwa kupumua lakini akaongezea kwamba anaugua pumu.
Msemaji wa polisi wa eneo la Yonkers aliiambia Newsbeat kwamba maafisa walimpata mtu mwenye umri wa miaka 45 ndani ya gari.
Wafanyikazi wa Ambiulensi walimpatia dawa inayoitwa Narcan ili kumuokoa na baadaye alipelekwa hospitalini mda mchache baadaye.
Satish Palav,meneja wa usiku wa mgahawa wa Ramada inn huko Yonkers alithiibitishia Newsbeat kuwa DMX alikuwa akiishi hapo.
''Baadaye ambiulensi iliwasili na kuja kumchukua''.
Alisema kuwa mwanamuziki huyo aliingia katika hoteli hiyo tarehe mosi mwezi Februari lakini hajarudi tangu alipopelekwa hospitalini.
0 maoni:
Chapisha Maoni