February 10 stori kutoka Shinyanga walikoweka kambi timu ya wekundu wa MsimbaziSimba wakisubiri mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya klabu ya Stand United, zimeandikwa stori mpya kuhusu kiungo wa timu hiyo kufikishwa kituo cha polisi, kiungo wa SimbaMwinyi Kazimoto ameripotiwa kufikishwa kituo kikuu cha polisi Shinyanga.
Mwinyi Kazimoto amefikishwa kituo kikuu cha polisi mkoani Shinyanga, kwa tuhuma za kumpiga mwandishi wa habari wa gazeti la MwanaSpoti Mwanahiba Richard, Kazimotoanayedaiwa kufanya kosa hilo kutokana na kudai kuwa mwandishi huyo aliwaandika vibaya kuwa wachezaji wa Simba waliocheza mechi ya Prisons na Mbeya City walikuwa chini ya kiwango na wanapaswa wachunguzwe kwa maana ya kuwa wamepewa rushwa.
Hivyo baada ya mazoezi ya Simba yaliofanyika uwanja wa Kambarage mkoaniShinyanga ndio inaripotiwa Kazimoto alitenda kosa hilo, bado Kazimoto na viongozi waSimba hawajapatikana kuzungumzia chochote juu ya tuhuma hizo, Mwanahiba aliriripoti katika kituo cha polisi na kupewa hati ya mashitaka (RB) yenye nambaSHY/RB/895/2016, fomu ya matibabu (PF3) kisha akapelekwa hospitali kwa matibabu.
0 maoni:
Chapisha Maoni