February 9 jina la Lionel Messi
linagonga vichwa vya habari za michezo kwa awamu mbili sasa, baada ya
awali kuripotiwa kuwa anafanyiwa uchunguzi wa tatizo la figo, good
news iliyonifikia kutoka 101greatgoals.com kuhusu mchezaji huyo mwenye tuzo tano za Ballon d’Or anaripotiwa kuwa na mpango wa kununua gari la kifahari.
Licha ya kuwa Lionel Messi huwa sio mpenzi sana wa magari ya kifahari kama ilivyo kwa mpinzani wake Cristiano Ronaldo, safari hii kuna tetesi kuwa anapanga kununua 1957 Ferrari 335 S Spider Scaglietti, gari ambalo linatajwa kuwa na thamani ya euro milioni 32 zaidi ya bilioni 78 za kitanzania.
0 maoni:
Chapisha Maoni