HUU NDIYO MUDA AMBAO ZOUMA ATAKAA NJE KUUGUZA MAJERAHA
-Beki wa Chelsea Mfaransa Court Zouma atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi sita baada ya kuumia vibaya katika pambano dhidi ya Manchester United, Vipimo vilivyofanywa na madaktari wa Chelsea vinaonesha kuwa Mfaransa huyo ameumia msuli wa nyuma ya goti ambao kimsingi unamfanya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu cha miezisita.
Kutokana na taarifa hizo ni wazi sasa Kurt Zouma atakosa michezo ya Euro itakayofanyika katika ardhi ya nyumbani kwao nchini Ufaransa lakini pia atakosa michezo yote ya Chelsea iliyobaki msimu huu.
Tayari taratibu za kufanyiwa upasuaji zimeshaandaliwa na madaktari wa Chelsea baada ya kujua kiwango cha majeraha ya Zouma na tayari klabuya Chelsea imetoa tamko kupitia mtandao wa klabu hiyo www.chelseafc.com
Taarifa ya klabu inasema “Kurt atafanyiwa upasuaji ndani ya masaa 48 yajayo na anatarajiwa kuwa nje kwa kipindi kinachokadiriwa miezi sita”.
Kurt Zouma kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter ameandika “nitarejea nikiwa kamili. Asanteni kwa mesejizenu”.
Kutokana na taarifa za kuumia kwa Kurt Zouma kuwasili mapema kuna uwezekano Chelsea wakafikiria kuhusu uwezekano wa kumuongezea mkataba nahondha wa Klabu hiyo John Terry ili aendelee kukipiga Stamford Bridge.
0 maoni:
Chapisha Maoni