Mlinzi wa Ghana Jonathan Mensah amejiunga na Anzhi Makhachkala katika mkataba wa miaka miwili u nusu.
Mlinzi
huyo wa Black Stars mwenye umri wa miaka 25 alikuwa akiichezea Evian
Thonon Gaillard katika mkataba uliofaa kukamilika mwisho wa msimu.Atajiunga na Anzhi Makhachkala mwishoni mwa msimu wa baridi.
Mensah alikuwa miongoni mwa kikosi cha timu iliyoshinda kombe la dunia la vijana mwaka wa 2009.
Vilevile aliichezea Black Stars katika kombe la dunia mwaka wa 2010 na 2014.
Vilevile alikuwa katika timu iliyoiwakilisha Black Stars katika mashindano ya ubingwa wa Afrika mwaka wa 2010 na 2015.
0 maoni:
Chapisha Maoni