Kiungo wa klabu ya
Yanga Thaban Kamusoko amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya
Tanzania kwa mwezi disemba, 2015 baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa
yanga Amissi Tambwe
Kamusoko ameisaidia timu yake katika michezo
iliyochezwa mwezi disemba kwa kushiriki dakika zote katika michezo
mitatu iliyochezwa mwezi wa disemba.kwa kuchaguliwa kwake kuwa mchezaji bora wa wa mwezi disemba, atakabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa ligi.
0 maoni:
Chapisha Maoni