Uongozi wa bodi ya
mchezo wa tenesi ulimwenguni, umethibitisha kwamba mwamuzi wa mchezo huo
amefungiwa kuchezesha mchezo huo na mwingine vyeti vyake vinashikiliwa
na kupewa adhabu ya mwaka mmoja kutojishirikisha na mchezo huo.
Uamuzi
huo umetolewa kutokana na kuhusishwa na masuala ya rushwa , lakini kama
hiyo haitoshi maofisa wengine wanne wamesimamishwa kwa muda
usiojulikana huku uchunguzi dhidi yao ukiendeshwa.Mwamuzi huyo amefungiwa maisha kujishirikisha na mchezo huo, na inaelezwa kuwa mnamo mwezi February mwaka 2015 Kirill Parfenov, mwenye uraia wa Kazakhstan alipatikana na hatia ya kufanya mawasiliano na ofisa mwingine kupanga matokeo ya mchezo uliokuwa mbele yao.
Mwezi uliopita mamlaka ya mchezo wa tenisi iliamua kufanya mapitio ya harakati zake za kuzuia rushwa mchezoni kufuatia madai kwamba ushahidi wa upangaji mechi haukufuatwa .
0 maoni:
Chapisha Maoni