
Shirikisho la Mpira
wa Kikapu ( NBA) litazindua rasmi msimu wa kwanza wa ligi ya mpira wa
kikapu kwa vijana kwenye kituo cha vijana cha Michezo cha Jakaya Mrisho
Kikwete jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 27 Februari mwaka huu.
Sherehe
hii ya ufunguzi wa mashindano hayo itahudhuriwa na Mchezaji Nyota wa
mchezo huo na Mwandamizi wa shirikisho la Mpira wa kikapu Ulimwenguni
Allison Feaster utakuwa ni uzinduzi rasmi wa ligi ya Mpira wa Kikapu kwa
Vijana wenye umri kati ya miaka 12 na 14.Ligi hii itajumuisha shule zipatazo thelathini (30) kutoka maeneo ya karibu na kila shule ikiwakilisha moja wapo ya timu 30 zinazoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani.
Ligi ya mpira wa kikapu ya vijana (Jr. NBA League) ni ligi ya NBA ya dunia inayoshirikisha mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana, wavulana kwa wasichana na inafundisha stadi za msingi za mchezo wa mpira wa kikapu pamoja na maadili muhimu ya mpira wa kikapu kwa wachezaji wanaoanza, Lengo likiwa ni kusaidia kukuza na kuboresha uzoefu wa Wachezaji, Makocha na Wazazi.
0 maoni:
Chapisha Maoni