Manchester United kumkosa De Gea tena

De GeaDe Gea aliumia akijiandaa kwa mechi dhidi ya FC Midtjylland nchini Denmark 
 
Klabu ya Manchester United itakuwa bila kipa David de Gea kwa mechi ya tatu mfululizo itakapowakaribisha nyumbani vijana wa FC Midtjylland kutoka Denmark mechi ya Europa League leo jioni.
De Gea hajacheza mechi mbili tangu aumie goti akipasha misuli moto kabla ya mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya FC Midtjylland wiki iliyopita nchini Denmark.
United walilazwa 2-1.“Hatacheza, hilo nina uhakika nalo,” amesema meneja wa Manchester United Louis van Gaal.
Winga Antonio Valencia anakaribia kuwa sawa kucheza lakini hataweza kucheza leo pia.
Valencia hajacheza tangu afanyiwe upasuaji mguuni Oktoba.
Beki Chris Smalling atachunguzwa baada ya kugonga ubao wa matangazo wakati wa mechi ya Kombe la FA dhidi ya Shrewsbury Jumatatu, mechi ambayo United walishinda.
Donald Love huenda akachezeshwa tena huku naye Marcos Rojo akitarajiwa kuchezeshwa dakika 20.
Mshambuliaji Wayne Rooney, kiungo wa kati Marouane Fellaini na beki Matteo Darmian bado wanauguza majeraha.
Van Gaal amesema United watakuwa “wabunifu sana” kujaribu kulipa deni la mechi ya mkondo wa kwanza na kuondoka na ushindi.
“Lazima tufunge, hilo ni wazi. Lazima tuwapangue na kwa hivyo itabidi tuwe wajanja sana,” ameongeza.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni