
Kuwasili kwake mjini Cairo kunamaanisha kuwa mahasimu wa jadi katika ligi kuu ya Misri Ahly na Zamalek wote wanamakocha wapya.
Zamalek majuzi tu walimsajili kocha mpya Alex McLeish.
Kwa sasa Jol anawasili Ahly wakiwa kileleni mwa jedwali la ligi kuu ya Misri wakifatwa kwa karibu na mabingwa watetezi Zamalek.
Mbali na kuifunza Tottenham na Fulham, Jol vilevile ameifunza vilabu vya Ujerumani Hamburg na Ajax Amsterdam ya Uholanzi.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 amekuwa akishabikia mechi kupitia kwa runinga baada ya kibarua chake kuota nyasi mwaka wa 2013 alipofutwa kazi na Fulham.
0 maoni:
Chapisha Maoni