
Jose Mourinho ndiye
afaaye zaidi kusaidia Manchester United kukabiliana vilivyo na
Manchester City watakaokuwa chini ya Pep Guardiola msimu ujao, haya kwa
mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Porto Benni McCarthy.
BBC
imefahamu kwamba huenda Mourinho, 53, aliyekuwa meneja wa Chelsea,
huenda akateuliwa kumrithi Louis van Gaal kama meneja Old Trafford
majira yajayo ya joto.McCarthy, 38, alicheza chini ya Mourinho raia huyo wa Ureno alipokuwa mkufunzi wa Porto.
"Mourinho ni mmoja wa watu wanaojua jinsi ya kumshinda Guardiola na mbinu zake,” ameambia BBC Sport.
- Manchester United yazungumza na Mourinho
- Van Gaal akanusha uvumi kuhusu Mourinho
- Guardiola kuwa meneja Manchester City

Guardiola, alikuwa kocha wa Barcelona, kwa sasa ni mkufunzi mkuu wa Bayern Munich.
Klabu ya Manchester City ilitangaza majuzi kwamba atamrithi Manuel Pellegrini majira yajayo ya joto.

Alifutwa kazi miezi saba tu baada ya kuongoza klabu hiyo kushinda Ligi ya Premia.
Alikuwa Chelsea kwa kipindi cha kwanza 2004-2007.
0 maoni:
Chapisha Maoni