Mwenyekiti wa
klabu inayocheza ligi ya daraja ya chini nchini Kenya Nicholas Mwendwa
ameteuliwa kuwa rais mpya wa shirikisho la soka Kenya (FKF).
Bw Mwendwa amechaguliwa kwenye uchaguzi wa taifa wa shirikisho hilo ambao ulifanyika Kasarani, Nairobi.Aliungwa mkono na wajumbe 50 kati ya wajumbe wote 77 na kuwashinda Bw Ambrose Rachier na Ssemi Aina.
Aliyekuwa rais kwa miaka minne, Bw Sam Nyamweya, alijiondoa kutoka kwenye uchaguzi muda mfupi kabla ya kura kupigwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni