Mtoto Ilham Mohamed
ARUSHA: Hujafa
hujaumbika! Mtoto Ilham Mohamed 19, (pichani) mkazi wa Ngarenaro
jijini hapa amezaliwa akiwa na ulemavu wa viungo kiasi cha kumfanya
aonekane mtoto mdogo, lakini bibi wa mtoto huyo, Zuleha Ismail
anacholalamikia ni kitendo cha mama Ilham, Sapna Parakash kumtelekeza
mwanaye.
Mtoto huyo akiwa na bibi yake, Zuleha Ismail
BIBI WA MTOTO NDIYE MWENYE KISA
Akizungumza kwa masikitiko na gazeti
hili mwanzoni mwa wiki hii nyumbani kwake, Ngarenaro, bibi Ilham alisema
alitelekezewa mtoto huyo mwaka 1997 na mama yake kwenda kuishi na
mwanaume mwingine baada ya kuachana na mtoto wake aliyemtaja kwa jina la
Mohammed Ismail.
Mama Ilham, Sapna Parakash
MSIKIE MWENYEWE
“Mama wa mtoto huyu amenitelekezea hapa.
Aliwahi kuja mara moja lakini hakutaka kumshika wala kumbeba.
Alimwambia ambariki ili apate mdogo wake kwani licha ya kutafuta tiba na
mwanaume aliyenaye lakini ameshindwa kupata ujauzito.”
AELEZEA NDOA YA SAPNA NA MWANAYE
Bibi huyo alisema kuwa, Sapna aliolewa na mtoto wake, Mohammed ambaye aliigiza kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu.
“Baada ya kujifungua mtoto mwenye
ulemavu, nahisi aliona kama laana, akaamua kumtelekeza kwangu yeye
akaenda Dar. Nasikia akaolewa na mwanaume mwingine na sasa hivi yupo nje
ya nchi.”
ALIKUWA NA MIEZI 3
“Aliniachia Alham akiwa na miezi 3. Sasa
hivi ana miaka 19. Nimetumia fedha nyingi kumtibu maradhi aliyonayo.
Ana mtindio wa ubongo uliosababisha miguu kukosa nguvu ya kusimama,
mgongo kupinda na shingo kuzunguka bila mpangilio.”
MATIBABU YAKE NI INDIA
“Niliwahi kumpeleka hospitali moja ya
hapa Arusha, daktari bingwa wa magonjwa hayo akaniambia, Ilham anatakiwa
kwenda kufanyiwa upasuaji nchini India. Kwa hiyo niandae kiasi cha
shilingi milioni 24.
“Nimekuwa nikitumia shilingi 50,000 kila
wiki kumnunulia dawa. Kwa kipindi chote hadi kufikia leo hii,
nimeshatumia pesa nyingi na sasa hivi sina kitu jamani,” alisema bibi
huyo.
Amani lilimpigia simu baba wa mtoto
huyo, Mohammed ambaye alisema: “Ni kweli Ilham ni mwanangu. Mama yake
sijui hata alipo. Mimi hali yangu kipesa ni mbaya, sina kitu.”
ALIYEGUSWA NA HABARI
Kwa mwenye kuguswa na habari ya bibi
Ilham na anataka kunmsaidia mtoto huyo anaweza kuwasiliana naye kwa
kutumia namba; 0754568378 au 0622300250.
0 maoni:
Chapisha Maoni