Staa wa Bongo Muvi, Flora Mvungi na ‘kibendi’ chake.
DAR ES SALAAM:
Makubwa! Ikiwa mtoto wake wa pili akiwa angali na umri wa miezi 6, staa
wa Bongo Muvi, Flora Mvungi tayari amenasa ‘kibendi’ kingine huku
akiwaomba watu ambao wanamshangaa wamuache kama alivyo.
Akizungumza
na gazeti hili, Flora ambaye kwa hivi sasa ana watoto wawili; Tanzanite
na Africa, amewataka watu waache kumjadili kwani hakuna ambaye
anamsaidia kulea na ukizingatia watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.
“Hivi jamani kwa nini watu wanapenda
kufuatilia maisha ya watu? Mimi hata kama nikizaa watoto kumi hakuna
ambaye ananisaidia kulea, waniache nizae maana hawanisaidii kulea, mimi
na mume wangu tumepanga kuzaa kadiri tunavyoweza,” alisema Flora.
Staa huyo alizidi kufunguka kuwa, mimba
aliyonayo iliingia bahati mbaya na hawezi kuitoa hata siku moja na ni
bora azae, amalize na aweze kufanya vitu vingine vya maendeleo.
“Nafikiri watu wanataka nikipata
ujauzito nitoe kitu ambacho siwezi kukifanya kabisa ni bora nikazaa
kisha nipumzike ili niweze kuendelea na maisha mengine,” alisema Flora.
0 maoni:
Chapisha Maoni