Mwasiti: Mimi siyo kabinti, mwaka huu nazaa!

Mwasiti-3
Mwasiti
Makala:Imelda Mtema
UKIZUNGUMZIA kati ya ‘vichwa’ vya kike vilivyotikisa na vinavyoendelea kutikisa ndani ya Jumba la Vipaji (THT) ni wazi utamtaja, Recho ‘Kizunguzungu’ Linah, Alice pamoja na mwanadada Mwasiti.
Mwasiti amejaaliwa sauti ya kipekee inayomfanya kila shabiki anayesikia nyimbo zake lazima ampe ‘saluti’. Showbiz Xtra ilipata wasaa wa kuchonga naye mawili-matatu kama makala haya yanavyo-jieleza;
Xtra: Tupe siri ya wimbo wako mpya wa Sema Nae
Mwasiti: Wimbo huu nimeutoa ikiwa ni maalum kuwapa mashabiki zangu nafasi ya kujua umuhimu wa kuongea mambo yao kiundani zaidi na siyo kuyatoa nje. Ilikuwa kuwaambia watu mtu na mke wake kwamba vitu vyenu ongeeni nyie wenyewe, kwa sababu sasa hivi wengi wenye matatizo hushindwa kuwafikia watu wao kwa kuogopa kuwapoteza hivyo kuishia kuwaambia marafiki zao ama watu wao wa karibu.
Xtra: Kwa nini unaficha uhusiano wako?
Mwasiti: Ahaa haaa! Kwanza huwa siamini kabisa kama kuwaonesha watu mpenzi wako ni kupata umaarufu zaidi ama utasifiwa. Ni kweli naficha na ni muda mrefu sana nimeamua kuwa hivi kwamba uhusiano wangu utabaki kuwa siri na kama watu wanataka kunijua kiundani kwanza wanijue zaidi kimuziki.
Xtra: Una mpango wa kuzaa sasa?
Mwasiti: Well! Nimekuwa nikiulizwa sana kuhusu kuzaa, kila kona swali ni hilohilo, wengi wanatamani kujua nitazaa lini, kikubwa Mwenyezi Mungu akijalia mwaka huu au ujao nitazaa. Hakuna mwanamke asiyetamani mtoto na mimi siyo kabinti ni mdada kwa sababu nina boyfriend na nina uwezo wa kupata mtoto.
Xtra: Nasikia nyimbo zako zote unaandikiwa?
Mwasiti: Siwezi kukataa kwamba siandikiwi nyimbo. Ni kweli kuna baadhi ya nyimbo naandikiwa na nyingine naandika mwenyewe. Kwa mfano Nalivua Pendo nimeandikiwa na Barnaba, Mapito ameandika Amini, Serebuka pamoja na huu wa sasa wa Sema Nae nimeandika mwenyewe.
Xtra: Kwa nini unapenda kuandika nyimbo za mapenzi?
Mwasiti: Kuandika nyimbo za mapenzi sidhani kama ni tatizo. Kuwapa nafasi watu wapate ujumbe kupitia nyimbo zangu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni