Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Taasisi binafasi
ya Karibu Tanzania Association (KTA) kwa pamoja wamezindua programu ya
maendeleo ya soka kwa wanawake vijana ili kuhamasisha usawa wa kijinsia,
uwezeshaji kijamii na kiuchumi kwa wanawake nchini itakayofadhiliwa na
Shirika la Forum Syd kutoka nchini Sweden.
Uwekaji
saini wa mkataba huo wa ushirikiano umefanywa na Katibu Mkuu wa TFF,
Mwesigwa Selestine na Mia Mjengwa Bergdahl, Mratibu wa Programu hiyo
kutoka taasisi ya Karibu Tanzania Sweden katika ofisi za TFF zilizopo
Karume.
Programu
hiyo ni ya aina yake ambayo haijapata kufanyika nchini inalenga kujenga
mfumo utakaotumiwa nchi nzima katika kutoa elimu na mafunzo kwa soka la
wanawake kwenye maeneo ya ufundi (makocha), waamuzi (refarii), uongozi
na tiba kwenye michezo.
Pia
itawezesha kuendeleza vipaji kwa wachezaji wanawake vijana na kuongeza
hali ya kujitambua na kujiamini kwa walengwa. Lengo ni kuongeza idadi ya
wachezaji wenye ubora na viwango kwa soka la wanawake vijana katika
ngazi zote, hivyo kuifanya programu hii kuwa nyenzo katika kuwawezesha
wanawake.
Kwa
kuanzia kozi 20 za soka la wanawake vijana kwenye Vyuo 20 vya maendeleo
ya wananchi zitaanzishwa kwenye kanda saba. Jumla ya wanawake vijana 600
ikiwamo 30 kutoka katika kila chuo cha Maendeleo ya Wananchi
watashiriki.
Katika
programu hii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto wanashiriki kikamilifu kwa kuwezesha wanafunzi na miundo mbinu ya
vyuo vya maendeleo ya wananchi vilivyo chini ya wizara hiyo kutumika
katika kufanikisha programu hii.
Mafunzo
yatatolewa sambamba na mafunzo mengine ya kawaida yanayotolewa kwenye
Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi, kama vile maarifa ya jumla na mafunzo ya
ufundi.
http://tff.or.tz/.../355-tff-kta-zazindua-programu-ya-maendel...
0 maoni:
Chapisha Maoni