Van Gaal: Itabidi tushinde Europa League

Van GaalImage copyrightPA
Image captionManchester United kwa sasa wamo nambari sita ligini
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema njia rahisi sasa kwa klabu hiyo kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao ni kushinda Europa League.
Manchester United walishindwa 2-1 ugenini Sunderland Jumamosi na sasa wamo alama sita nyuma ya klabu nne zinazoongoza Ligi ya Premia.
Alipoulizwa baada ya mechi hiyo iwapo kuna matumaini kwa United kumaliza katika nafasi nne za kwanza, Van Gaal alisema: “Itakuwa vigumu sana.
“Baada ya mechi hii, nao njia bora zaidi kwetu ni kushinda Europa League lakini pia haitakuwa rahisi kwa sababu kuna timu nyingi nzuri huko.”
Tangu msimu uliopita, washindi wa Europa League wamekuwa wakizawadiwa nafasi ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wakiingia hatua ya kufuzu kabla ya hatua ya makundi au hatua ya makundi.
Van Gaal hata hivyo amesema hajapoteza matumaini ya kumaliza katika nne bora ligini.
United watacheza mechi ya mkumbo wa kwanza Europa League hatua ya 32 bora dhidi ya klabu ya Denmark FC Midtjylland Alhamisi.
Watakutana na Shrewsbury katika Kombe la FA wikendi ijayo. Mechi yao ijayo Ligi ya Premia itakuwa tarehe 28 Februari dhidi ya Arsenal uwanjani Old Trafford
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni