Beki wa Manchester City Martin Demichelis anatuhumiwa na chama cha soka nchini England (FA) kujihusisha na masuala ya ku-bett.
Taarifa iliyotolewa na FA inasomeka kwamba: “anatuhumiwa kwa kukiuka kanuni na sheria za FA zinazosimamia mchezo wa soka kati ya 22 January 2016 na 28 January 2016.”
Demichelis ambaye ameitumika Manchester City kwenye michezo 29 msimu huu, amepewa muda hadi April 5 kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
Sheria ya kuwazuia ku-bet wale wote wanaohusika na masuala ya soka ilianza kutumika August 1, 2014 duniani kote.
Demichelis ameuambia mtandao wa ESPN kuwa atakuwa na mengi ya kuzungumza baada ya kukutana na viongozi wa klabu yake.
“Ni kawaida siwezi kuzuia tuhuma hizo, lakini naamini kila mtu anaelewa hilo, nitakuwa tayari kuzungumza zaidi baada ya kukutana na mwanasheria wa klabu,” alisema.
“Sidhani kama ni jambo kubwa ni kitu ambacho kinaweza kutatuliwa kwa haraka”
Sheria inawazuia wote wanaohusika na mchezo wa soka kubet kwa namna yeyote ile au kutoa maelekezo, kuruhusu, kusababisha au kumuwezesha mtu yeyote kubet juu ya (i) matokeo, maendeleo, matukio ya mchezo wa soka au mashindano au (ii) jambo lolote linalohusiana na mchezo wa soka mahali popote duniani kwa mfano uhamisho wa wachezaji, ajira za makocha, uteuzi wa vikosi au mambo ya kinidhamu.
Wachezaji pia wanazuiwa kutoa taarifa za ndani kwa mtu yeyote kwa lengo la kubet au ku-support vitendo vya kubet.
City bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo lakini ripoti zinadai kwamba tuhuma hizo hazihusiani na ushawishi ambao Demichelis alikuwa nao kwenye mechi hizo.
Demichelis amesema anaelewa kwamba taratimu na kanuni haziko sawa kwenye ligi zote.
“Mambo yako tofauti kila sehemu”, aliiambia ESPN. Hispania jambo hili linaruhusiwa (kubet kwenye mechi ambazo haziihusishi timu yako), au iwe imezuiwa kwa sasa. Lakini nikipata taarifa kutoka kwa wanasheria nitazungumza mengi zaidi kuliko sasa. Sina tatizo kuhusu kusema ukweli, sina cha kuficha.
0 maoni:
Chapisha Maoni