Zikiwa zimebaki siku 3 kuelekea mchezo wa El Clasico – Barcelona vs Real Madrid, leo nakuletea mambo matano muhimu kuelekea mchezo huu mkubwa kwa ngazi ya vilabu duniani.
1. Timu gani inaingia kwenye El Clasico ikiwa kwenye hali nzuri ya kimchezo.
Barcelona wanaingia kwenye mchezo wakiwa vizuri zaidi ya wapinzani wao – wapo kwehye rekodi ya kutofungwa katika mechi 39, hivyo wanaonekana kuwa vizuri kuwazidiLos Blancos. Lakini Barca wana wasiwasi mkubwa na wachezaji wao watatu muhimu wanaounda ‘MSN’ wanasafiri kutoka America ya Kusini kurudi Spain – uchovu unaweza kupunguza fitness yao kuelekea mchezo huu.
Barcelona wanaingia kwenye mchezo wakiwa vizuri zaidi ya wapinzani wao – wapo kwehye rekodi ya kutofungwa katika mechi 39, hivyo wanaonekana kuwa vizuri kuwazidiLos Blancos. Lakini Barca wana wasiwasi mkubwa na wachezaji wao watatu muhimu wanaounda ‘MSN’ wanasafiri kutoka America ya Kusini kurudi Spain – uchovu unaweza kupunguza fitness yao kuelekea mchezo huu.
Kwa upande wa kikosi cha Bwana Zinedine Zidane, wachezaji wake muhimu wamepata mapumziko ya kutosha baadhi yao, Gareth Bale na Benzema hawakushiriki kwenye mechi yoyote ya kimataifa wikiendi iliyopita – Pia Madrid wataingia kwenye mchezo wakitoka kupata matokeo chanya katika mchezo mgumu dhidi ya Sevilla katika mechi yao ya mwisho ya La Liga kabla ya mapumziko.
2. Ushindi Utamaanisha nini kwa mshindi wa El Clasico
Ushindi kwa upande wa Barcelona itakuwa wameweka rekodi ya kucheza mechi 40 mfululizo bila kupoteza na pia Zidane atakuwa kafeli mtihani wake mkubwa akiwa kocha wa Real. Alifaulu mtihani wake wa kwanza kuiwezesha Madrid kuiondoa Roma kwenye 16 bora ya UEFA, lakini kipigo kitatoa majibu kwamba Los Blancos ni wanyonge wa Barca ndani ya Spain bila wamebadilisha makocha mara ngapi.
Ikiwa Real watashinda, hali ya kujiamini itapanda katika mji mkuu wa Spain. Kutakuwepo na mazungumzo juu ya mkataba mpya kwa Zizzou na watapata kujiamini kwamba hakuna wa kuwazuia kutwaa ubingwa wa 11 wa mabingwa wa ulaya msimu huu.
Sare itawanufaisha pande zote mbili, Barca wataendelea kuwa na rekodi yao ya kutokupoteza mechi ya 40 mfululizo na pia Madrid wakinufaika kuelekea mwishoni mwa msimu wa La Liga.
3. Ni namna gani Madrid wanaweza kuiangamiza Barca?
Kasi ya Bale na Ronaldo, na kinda Lucas Vazquez kutokea benchi, utakuwa msingi mkuu wa silaha za Real Madrid vs La Blaugrana. Barcelona mara zote hutoa nafasi kwa wapinzani kuchezea mpira kwenye nusu yao ya uwanja na mchezo huu hautokuwa na tofauti.
Lakini inabidi timu pinzani ziwe na uwezo wa kukaa na mpira ili uweze kuchezea mpira kwenye nusu ya uwanja ya Barca – kikosi cha Rafa Benitez kilichodhalilishwa kwenye raundi ya kwanza ya La Liga msimu huu kilishindwa kufanikisha hilo. Madrid watahitaji kuhakikisha kutafuta mbinu ya kuzuia Sergio Busquest asiumiliki mchezo ikiwa watataka kupata matokeo chanya – wakipoteza umiliki wa sehemu ya kiungo basi hali itakuwa ngumu kwao.
4. Ni namna gani Barca wanaweza kuiangamiza Madrid?
Safu ya kiungo inaendelea kuwa udhaifu mkubwa kwa Madrid ambao Barca waliutumia mechi iliyopita na huenda wakautumia tena Jumamosi hii. Casemiro atafaa zaidi kucheza kiungo cha kukaba kuliko Toni Kroos lakini kwenye mchezo uliopita dhidi ya Roma hakuonekana kuwa sawa.
Kama Barca wakimshambulia sana basi na kumuweka kwenye presha basi anaweza kufanya makosa yatakayoigharimu timu. Udhaifu mwingine wa Madrid ambao Barca wanaweza kuutumia ni upande wa kushoto anapocheza Marcelo ambye mara nyingi amekuwa anakosa usaidizi sahihi kutoka kwa wenzie katika kumzuia Neymar anayetokea kulia mwa kiungo cha Barcelona.
5. Je hii ndio itakuwa Clasico ya mwisho kwa Ronaldo?
Mengi yatategemea na userious wa PSG kuhusu usajili huu. Kwa kelele zote za mchezaji na klabu yenyewe kwamba nahodha huyo wa Ureno ataendelea kuwepo Bernabeu mpaka mwisho mwa maisha yake ya soka, basi itabidi PSG wapeleke ofa ambayo Madrid na CR7 hawawezi kuikataa.
Real Madrid watatumia fedha Kwenye kipindi cha usajili kinachokuja ili kuimariaha kikosi chao chenye mapungufu kadhaa na hivyo watahitaji kuuza wachezaji ili kupata fedha za kuimarisha kikosi chao. Lakini pia wanaweza wasimuuze Ronaldo na panga likawaangukia Isco na James Rodriguez ambao wamekuwa na msimu usiovutia.
6. Je hii inaweza kuwa El Clasico ya kwanza na ya mwisho kwa kocha Zinedine Zidane.
Kipigo cha 4-0 walichopata Madrid El Clasico ya kwanza msimu huu ndio kilipigia mstari wa mwisho ya ajira ya Rafa Benitez msimu Santiago Bernabeu. Na ikiwa Madrid atafungwa kipigo kizito tena basi – wale wanachama wa Madrid ambao Zidane hana uwezo wa kuiongoza timu hiyo watapata silaha za kutumia kumuondoa. Lakini msingi mkubwa wa ajira ya Zidane upo kwenye michuano ya ulaya. Ikitokea akashinda UCL, atasamehewa hata kama Los Blancos wakifungwa 10-0 jumamosi hii.
0 maoni:
Chapisha Maoni