Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameongoea na Sky Sport kuhusu mbio za ubingwa msimu huu kwa jinsi ulivyo sasa hivi.
Kocha Ferguson ameshinda mataji 13 kwenye muda wa miaka 26 aliyokaa ndani ya Old Trafford, hivyo maneno yake kuhusu chochote cha EPL lazima kichukuliwe serious.
Sir Ferguson anasema Tottenham Hotspurs ndio timu pekee yenye uwezo wa kuizuia Leicester City kwenye mbio za ubingwa. Ferguson amesema “Leicester wanakaribia kwenye mstari wa kumaliza kama mabingwa, hiyo ni task kubwa sana kwao. Wanatakiwa kuwa hivi hivi hadi mwisho na hawatakiwi kibadirika, wanatakiwa kuwa hivi hivi kama walivyokua kwa miezi 6 iliyopita”.
“Naiona Spurs pekee kuwa ni ya hatari kwa Leicester City. Spurs kwa sasa wanacheza soka zuri zaidi ya miaka mingi niliowajua kwa miaka kadhaa iliyopita. Leicester wamekua timu bora kwa msimu mzima na wanastahili kushinda ubingwa.”
0 maoni:
Chapisha Maoni