El Clasico: Wengi wanaipa Barca nafasi lakini historia inaipa nafasi Madrid

Siku 4 kabla ya dunia ya wapenda soka kushuhudia mtanange wa wapinzani wa jadi wa soka la Hispania – FC Barcelona vs Real Madrid – nitakuwa nakuletea taarifa muhimu kila siku mpaka siku ya mchezo huo.
  Leo tuangalie historia – takwimu zinaonyesha Barcelona huwa wanapata taabu sana kupata matokeo dhidi ya Los Blancos wakati wanapokuwa na faida ya kuongoza ligi kwa pointi nyingi mbele wa wapinzani wao. Barca wanapokuwa na uongozi wa zaidi ya pointi 9 mbele ya Madrid, historia inaonyesha huwa wanapata taabu kupata pointi mbele ya Madrid.
Ingawa makampuni mengi ya kamari na wadau wengi wa soka wanaipa nafasi ya Barca kuibuka na ushindi, historia inatupa picha tofauti ya matokeo. Na kama matokeo ya siku za nyuma ni ya kuyaangalia kuelekea mchezo huu – pale Wakatalunya wanapokuwa wanaongoza ligi mbele ya Madrid kwa pointi 9 au zaidi basi mchezo unaofuatia dhidi ya Los Blancos huishia kwa Barca kufungwa au kutoa sare. 
Barca kwa sasa wanaongoza ligi kwa pointi 10 mbele ya Madrid – Atletico wanashika nafasi ya pili  na Madrid wakishika nafasi ya 3 – katika El Clasico tatu zilizopita ambazo Barca alikuwa anaongoza ligi kwa tofauti ya pointi hizi basi matokeo huwa hayawi upande wao. 
 
Msimu wa 2012-13 | Pengo la pointi 14 | Real Madrid 2-1 Barcelona
Hii mechi ilikuja wakati kukiwa na pengo kubwa zaidi la pointi baina ya wapinzani hawa kuelekea El Clasico. Walikutana mnamo Mei 24 katika dimba la Bernabeu. Kikosi cha Barca chini Tito Vilanova/Roura kilifungwa 2-1, Karim Benzema na Ramos wakifunga magoli ya ushindi, mchezo ambao Ronaldo alianzia benchi. 
Kumbukumbu nyingine ya mchezo huu ni adhabu ya kadi nyekundu kwa golikipa Victor Valdes baada ya filimbi ya mwisho kwa kumwambia refa Perez Lasa  “You bottled it, you’re shameless”   
Msimu 2005-2006 | 11 points | Real Madrid 1-1 Barcelona
Huku ikiwa imebaki michezo 8 kabla ya ligi kumalizika, kikosi cha Frank Rijkaard cha Barca walikutana na Madrid @CampNou wakiwa na pointi 11 zaidi kwenye ligi. Florentino Perez alikuwa ameondoka kwenye kiti cha urais mwezi mmoja nyuma na klabu ikawa kwenye kipindi cha mpito – Lopez Caro akiliongoza benchi na Fernando Martin akikaimu kiti cha urais. 
Pamoja na matatizo waliyokuwa wanapitia Real Madrid, lakini bado walifanikiwa kuondoka na pointi moja  – huku mechi ikajaa malalamiko kwa refa aliyetoa penati ya utata kwa Barca huku akikataa ya wazi kabisa kwa Madrid. Robert Carlos alitolewa kwa kadi nyekundu. Lakini goli la kusawazisha la Ronaldo De Lima likaufanya mchezo uwe sare baada ya goli la penati la Ronaldinho. 
  
Msimu 1990-91 | 13 points | Real Madrid 1-0 Barcelona
Hakuna maelezo mengi kuhusiana na story ya mchezo huu ambao ulichezwa huku bingwa akiwa kashafahamika. Barcelona tayari walishakuwa mabingwa na Atletico akishika nafasi ya pili. Barcelona hii ndio ile ya Johan Cruyff ‘The Dream Team’ – na inakumbukwa kwamba mdachi huyo alisema alikuwa na furaha kuona timu yake ikipoteza mbele ya Madrid kila mwaka ili mradi tu wao wawe mabingwa. Akisema suala la heshima anayopewa bingwa ‘Guard of Honour’ kabla ya mchezo lilikuwa jambo zuri. 
Aldana ndio alifunga goli pekee kwenye mchezo huo huku Zubizarreta akiokoa penati ya Butragueno ambaye alimaliza akiwa mfungaji bora msimu huo.  
Ushindi wa kwa Barcelona wikiendi ijayo utaweka rekodi mpya na pia utawapa uongozi wa pointi 13 mbele ya wapinzani wao – ushindi kwa Madrid utarejesha matumaini ya kusbinda ubingwa kama Barca ataendelea kuteleza.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni