Na BABU MKUSA
Kikosi cha timu ya taifa maarufu kama ‘Taifa Stars’ kwa kipindi cha hivi karibuni kimekuwa kikiimarika kutokana na kujumuisha wachezaji wenye vipaji pamoja na ushindani wa namba katika kikosi tofauti na kipindi cha nyuma ambapo mtu ulikua na uwezo wa kupanga kikosi kinachoanza na ikawa hivyo.
Leo hii ukianza na upande wa walinda lango Tanzania wapo wengi wanaoonesha matumaini ya kupunguza tatizo la magolikipa miaka ijayo kutokana na umri wao na vipaji vyao kama tu watanzingatia kanuni za mpira Aishi, Shabani Kado, Ally Mustafa ‘Bartez’, Manyika Jr, Said Mohamed ni moja ya hazina kubwa hapa hakuna shaka ya magolikipa kwa miaka ijayo kutokana na umri walio nao kama tu watakua na jitihada katika soka.
Upande wa mabeki wa pembeni hakuna shaka maana vijana wengi wapo kwenye fomu nzuri ya kiushindani hata katika vilabu vyao wanaonesha kuwa wana nia na soka, pale Yanga kuna Mwinyi Haji na Juma Abdul hakuna asiyejua mchango wao ndani ya klub hyo ya Jangwani pia wapo timu ya taifa pia.
Simba kuna wachezaji wanaocheza nafasi hiyo kama Tshabalala na Kessy wakiendelea kucheza na jitihada walizonazo kwa sasa tuna uhakika wa kuwa na hazina kubwa katika timu yetu ya taifa katika nafasi hii achilia mbali Shomari Kapombe ambaye ni mzoefu.
Inaonekana wapo wa kuweza kurithi mikoba ya Kapombe, hata katika ligi nimeona baadhi ya mabeki wa pembeni wenye kucheza staili ya Kapombe ya kupandisha timu kwa kuwasaidia mawinga mfano nilifanikiwa kuangalia mechi ya Mgambo JKT na Toto Africans yule beki wa kushoto wa Toto Salum Chuku yupo vizuri na kama atazingatia na kuwa na malengo katika soka tutakuwa hatuna shaka na nafasi hii.
Tatizo kubwa lipo katika mabeki wa kati katika timu yetu ya taifa kwa kipindi kirefu tumekuwa tukiwategemea Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ lakini hivi karibuni Nadir katangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa sasa tuna baki na Yondani ambaye naye kutokana na umri anahitaji mrithi wake. Katika mechi ya Stars na Chad, mwalimu aliamua kumtumia Nyoni kama beki wa kati ilhali Nyoni hucheza beki ya pembeni lakini hata ukiangali kwenye benchi beki pekee wa kati alikua ni Mwantika.
Tukimwangalia Nyoni yupo kwenye timu muda mrefu pia na yeye kulingana na umri wake muda wowote na yeye anaweza ondoka timu taifa. Swali la kujiuliza nani ni mrithi sahihi wa Yondani na Cannavaro pale Stars?
Kipindi cha Maximo alikua akiwatumia Cannavaro na Salum Swedi huku Yondani na Morris Agrey wakiwa nje. Baada ya kuondoka kwa Swedi Yondani alikuja kuchukua mikoba ya Swedi. Sasa nani anaweza kuja kuziba pengo la cannavaro?
Wengi tulitegemea pengine Hassan Isihaka kuja kua nguzo muhimu lakini bado hajafika pale wengi walipo tarajia, kwa upande wa Agrey Morris umri nae sio rafiki kwake pamoja na Morad.
Tanzania bado tunatatizo la mabeki wa kati aina ya Cannavaro naona bado tunasafari ndefu katika kumpata Cannavaro mwingine angalia hata katika klabu ya Yanga bado Vincent Bossou hajafanikiwa kufikia uchezaji wa Cannavaro angalia katika gemu ya Yanga na Azam alikua akiruhusu Kipre atembee na mpira kirahisi tofauti na Nadir.
Tukubali bado tuna kazi kubwa kupata mabeki wa kuaminika wa kati. Kama leo Yondani akipata majeruhi nani anaweza kusimama pale katikati? Nafasi ya kiungo na ushambuliaji haina tatizo, kuna vijana wengi sana wanaonesha uwezo katika miaka ijayo. Angalia hata performance ya wachezaji wetu katika ligi kuu kwa wachezaji wa nafasi ya beki wa kati utagundua bado tunasafari ndefu ya kumpata Nadir mwingine japo bado inawezekana kama wachezaji wetu watazingatia nidhamu na mazoezi.
Nidhamu imekuwa tatizo kwa wachezaji wetu wengi na hupelekea kupotea kimchezo. Mwantika David kama atatulia na kupata namba katika kikosi cha Azam bado nina uhakika wa kuweza kuziba nafasi ya Nadir lakini siyo kuziba pengo lake.
Mfano nzuri ni timu ya taifa ya Uingereza imewachukua muda mrefu kuja kupata wachezaji wa aina ya Allan Shearer sasahivi safu yao ya ushambuliaji ndiyo inaanza kuimarika baada ya kipindi kirefu kwa kuwategemea Harry Kane pamoja na Vardy pia Lalana. Wapo wengi wanaoweza kucheza hiyo nafasi lakini si kwa kiwango cha Nadir.
0 maoni:
Chapisha Maoni