MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal hakuingizwa kwenye Video rasmi ya Klabu hiyo ya Promosheni ya Ziara ya Kabla Msimu mpya kuanza ya huko China Mwezi Julai.
Huko China, Man United itashiriki Mashindano ya International Champions Cup kwa kupambana na Mahasimu wao Man City na Vigogo wa Germany Borussia Dortmund kwenye Mechi zitakazochezwa Miji ya Beijing na Shenzen.
Van Gaal alishirikishwa kwenye Video kama hiyo ya Promosheni ya Ziara za Kabla Msimu mpya kuanza za Miaka ya 2014 na 2015 huko USA.
Kuachwa huku kwa Van Gaal kwenye Video hii muhimu kumetafsriwa kuwa ni ishara kubwa Mdachi huyo atang'olewa mwishoni mwa Msimu huu huku akibakiza Mwaka mmoja kwenye Mkataba wake.
Tayari zipo habari nzito kuwa aliekuwa Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ameshasaini Mkataba wa awali na Man United na anatarajiwa kuingia Ofisini Old Trafford Mwezi Juni.
0 maoni:
Chapisha Maoni