Europa:Jurgen Klopp kurudi Dortmund

Image copyrightReuters
Image captionJurgen Klopp
Mkufunzi wa kilabu ya Liverpool Jurgen Klopp atakutana na timu yake ya zamani Borussia Dortmund katika robofanili ya kombe la Europa.
Klopp mwenye umri wa miaka 48 aliondoka Dortmund msimu uliopita baada ya kuiongoza timu hiyo shinda mataji mawili ya Bundesliga na kufika katika fainali ya vilabu bingwa Ulaya.
Sevilla,ambayo inajribu kushinda kombe hilo kwa mara ya tatu itakabiliana na Athelitico Bilbao katika mechi inayoshirikisha timu zote za Uhispania.
Villareal pia kutoka ligi ya Uhispania itachuana na timu ya Czech Sparta Prague huku kilabu ya Ureno Braga ikikabiliana na Shakhtar Donetsk kutoka Ukraine.
Image copyrightGetty
Image captionDortmund
Mechi hizo za robo fainali zitachezwa mnamo tarehe 7 na 14 mwezi Aprili.
Liverpool itasafiri Dortmund katika awamu ya kwanza ya mechi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni