Mcheza tenisi Roger Federer anatarajia kurejea viwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti ikiwa ni mapema zaidi ya matarajio yaliyokuwepo, imepangwa kuwa atashiriki katika mashindano ya wazi ya Tenisi ya Miami wiki ijayo.
Federer mwenye miaka 35 akiwa nafasi ya tatu kwa ubora duniani, mwezi Januari mwaka huu alishindwa kufanya vizuri katika Michuano ya wazi ya Australia katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Novak Djokovic.
Federer alishinda taji la mashindano ya Key Biscayne mwaka 2005 na 2006, na mwisho alicheza mwaka 2014 na kufikia hatua ya robo fainali.
0 maoni:
Chapisha Maoni