1.RAFAEL DA SILVA
Beki huyu namba mbili ambaye amedumu katika timu hiyo kwa kipindi kirefu aliuzwa na meneja huyo wa manchester united ili apishe ujio wa beki mpya marteo darmian ambaye mpaka sasa ameonekana kuchemsha katika timu hiyo sasa beki huyo anakipiga katika timu ya olyimpic lyon
2.ROBIN VAN PERSIE
Mchezaji huyo ambae aliwahi kuchukua kiatu cha ufungaji bora katika ligi kuu ya uingereza mwisho wa msimu uliopita aliuzwa na meneja wa manchester united kwa matumaini ya kwamba atapata mshambuliaji atakae weza kuziba pengo lake lakini mpaka sasa hajapatikana mbadala wa kuziba pengo lake huku wayne rooney akicheza chini ya kiwango.Mshambuliaji huyu ameuzwa katika timu ya Fenerbance ya uturuki
3.JAVIER HERNANDEZ,CHICHARITO
Mshambuliaji huyu alikuwa mwiba sana hasa pale anapotokea substution, alikuwa mchezaji anaecheza kwa ustadi hasa pale anapokuwa na kipa lakini alipofika van gaal alionekana hana thamani na kuuzwa kwa bei rahisi katika timu ya ligi kuu ya ujerumani ambayo ni Bayern Levekusen
Ni kiungo bora sana ambaye klabu ya man united ilimnunua kutokea katika klabu ya BORRUSIA DORTMUND katika kipindi chake akiwa na man united alicheza kwa kiwango cha kawaida hivyo kupelekea kocha Van Gaal kumrudisha katika timu yake ya Dortmund na huko mpaka sasa ameweza kuwa mchezaji muhimu katika kisosi cha timu hiyo ya ujerumani
5.LUIS FABIO NANI
Ni winga mbaye alikuwa anafuata nyayo za mreno mwenzie cristiano ronaldo,maisha yake ndani ya Old Traford yalianza kuyumba mara baada ya kocha Ferguson kustaafu kufundisha soka ambapo alipelekwa katika klabu yake ya awali ya sporting lisbon kwa mkopo na baada ya kumaliza mkopo alirudi na kocha Van Gaal alimuuza katika klabu ya Fenerbance ya uturuki
6.ANGEL DI MARIA
Pia winga huyu ambaye msimu uliopita alishika nafasi ya pili katika ligi la uingereza kwa kuota assists 11 nyuma ya fabregas wa Chelsea lakini pamoja na uwezo wake lakini kocha huyo mdachi aliamua kumuuza kwa matajiri wa kifaransa PSG na pia ndiye aliyevunja rekodi ya kununuliwa kwa bei kali katika ligi ya uingereza maarufu kama barclays
na pia kocha huyo ameshindwa kuitimizia timu hiyo matakwa kwa kutoipa hata kombe moja hadi na inaonekana ndo utakuwa msimu wake wa mwisho kuifundisha timu hiyo kwa kumpisha mreno Jose Mourinho
0 maoni:
Chapisha Maoni