Good news kwa soka la Tanzania hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya taifa ya Chad wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 itakayofanyika Gabon.
Tayari kuna taarifa za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu yaMansfield Town ya Ligi daraja la pili Uingereza Abdillahie Yussuf anaripotiwa kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Chad utakaochezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam Jumatatu ya March 28.
Kama ulikuwa hujui Abdillahie Yussuf amelelewa na katika klabu ya Leicester City ya Uingereza ambayo kwa sasa inanyemelea ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza kwa kuongoza Ligi hiyo kwa kuwa na point 66 ikifuatiwa na Tottenham Hotspurs yenye point 61.
0 maoni:
Chapisha Maoni