Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars alfajiri ya March 25 iliwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage ukitokea Chad kwa kupitia Ethiopia. Taifa Starswaliwasili Dar Es Salaam na kupokelewa na mapokezi mazuri kutoka kwa kikundi cha ushangiliaji cha Taifa Stars Suporter pamoja na watu mbalimbali.
Taifa Stars itacheza mchezo wake wa pili wa marudiano na Chad Jumatatu ya March 28 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, baada ya mchezo wa kwanza kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 uliyochezwa jumatano hii Chad katika uwanja wa Idriss Mahamat.
0 maoni:
Chapisha Maoni