Jumapili ya March 13 Kombe la
FA nchini Uingereza limeendelea kama kawaida kwa vilabu kadhaa kushuka
dimbani kucheza mechi yake ya raundi ya sita ya michuano hiyo.
March 13 michezo ya Kombe la
FA Uingereza ilichezwa miwili, kwa klabu ya Arsenal kuchuana na klabu ya
Watford na kuishia kuambulia kichapo cha goli 2-1.
Baada ya hapo Man United
walifuatia kucheza mchezo wao wa raundi ya sita ya Kombe la FA dhidi ya
wagonga nyundo wa London klabu ya West Ham United, ambao nao kupitia kwa
Dimitri Payet dakika ya 68 waliifunga Man United, lakini Man United
walikuja juu na kuambulia sare ya goli 1-1 baada ya Anthony Martial
kusawazisha goli dakika ya 83
0 maoni:
Chapisha Maoni