Kwa mara ya kwanza klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ambayo inaongozwa na
kocha lakini inachezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana
Ally Samatta, imempa nafasi ya kuanza katika mchezo wa leo dhidi ya
klabu ya KV Oastende.
Samatta amepata nafasi hiyo ya kuanza mchezo wa leo March 13, ikiwa ni
zaidi ya mechi nne amekuwa akiichezea timu hiyo akitokea benchi. Baada
ya Samatta kuanza first eleven, alipachika goli la kwanza kwa timu yake
dakika ya 25 ya mchezo, lakini hilo pia ni goli lake la pili toka
ajiunge na KRC Genk.
0 maoni:
Chapisha Maoni