Misri wametoka salama Nigeria, kazi imebakia kwa Taifa Stars Septemba 2 2016


Bado kivumbi cha mataifa ya Afrika kuendelea kuwania nafasi ya kuelekea fainali zaAFCON 2017 Gabon kinaendelea, March 25 2016 hatua ya Makundi ya kuwania kufuzu michuano hiyo iliendelea kama kawaida.
Kwa upande wa watanzania walikuwa wanaangalia mchezo wa Kundi G kati ya Nigeriadhidi ya Misri, kwani hili ndio kundi waliomo pamoja na Chad, hivyo dua zao zilikuwa nikuomba mchezo huo umalizike kwa sare ya aina yoyote ile, ili kutoweka tofauti ya point nyingi dhidi ya timu hizo.
Nigeria ambao walikuwa na nafasi ya pili wakiwa na point nne sawa naTanzania wameshindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Misri licha ya kuwa walikuwa nyumbani, ila wameishia kuambulia sare ya goli 1-1, Nigeria walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 60 kupitia kwa Oghenekaro Etebo, ila Misri walisawazisha dakika ya 90 kupitia Mohamed Salah.
kundi
Huu ndio msimamo wa Kund G ulivyo kwa sasa
Kwa sasa Misri wanaendelea kuwa kileleni mwa Kundi G wakifuatiwa na Nigeria, lakini mtihani unabakia kwa timu ya taifa ya Tanzania ambayo inahitaji nafasi ya kushirikiAFCON 2017 Gabon, ila mchezo wake wa marudiano dhidi ya Nigeria Septemba 2 unatabiriwa kuwa utakuwa mgumu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni