Usitarajie kumuona Ibrahimovic Man United kama mambo yataendelea kuwa hivi …


March 25 starsport wamerudisha jina la Zlatan Ibrahimovic kwenye headlines za kutaka kujiunga na klabu ya Man United ya Uingereza akitokea Paris Saint Germain yaUfaransa. Jina la Zlatan safari hii limerudi katika tetesi hizo kwa tofauti kidogo.
Mabosi wa Man United wanatajwa kuongeza nguvu za kuwania saini ya staa huyo, ili kuvizidi vilabu vya Arsenal na Chelsea ambavyo vinamuwania pia, Mabosi wa Man United wanataka kumpa mshahara wa pound 250,000 kwa wiki na kumfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa zaidi Uingereza.
Stori ni kuwa inaripotiwa kuwa Zlatan Ibrahimovic ana mpango wa kutua Man United ila kama Louis van Gaal ataondoka Man United, Zlatan anatajwa kutamani kufanya kazi naJose Mourinho ambaye aliwahi kufundishwa nae akiwa Inter Milan.
470508
Zlatan na Jose Mourinho wakati wakiwa katika klabu ya Inter Milan
Zlatan anamaliza mkataba wake na PSG mwishoni mwa msimu huu, lakini amegoma kusaini mkataba mpya na PSG, hivyo hadi mwishoni mwa msimu huu anatajwa kuwa atatua katika klabu ya Ligi Kuu Uingereza, kati ya Chelsea, Arsenal hususani Man United.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni