MISRI YAJIWEKA PAZURI, RWANDA, BURUNDI ZAFANYA KWELI KUFUZU AFCON 2017

CAF Troph
Michezo ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika ilimeendelea kushika kasi huku timu za taifa za bara la Afrika ikipambana kuhakikisha zinapata nafasi ya kucheza michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya timu za taifa.
 matokeo ya michezo yote iliyopigwa siku ya Jumanne March 29, 2016.
Nigeria imejikuta ikishindwa kufurukuta mbele ya Mafarao wa Misri baada ya kutandikwa kwa bao 1-0 ugenini na kuipa timu hiyo ya Kaskazini mwa Afrika nafasi kubwa ya kufuzu kwa fainali zijazo za mataifa ya Afrika.
Mchezo huo wa G ambalo ni kundi la Stars, ulipigwa kwenye mji wa Alexandria, Misri siku kadhaa baada ya Nigeria kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Misri kwenye mchezo uliopigwa huko Nigeria.
Misri imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali hizo ikiwa inaongoza kundi G kwa pointi 7 ikifuatiwa na Nigeria yenye pointi mbili wakati Tanzania ikiwa bado mkiani kwa pointi yake 1.
Stars inahitaji kushinda mechi zake mbili zijazo kwa idadi nzuri ya magoli ili kujiweka kwenye nafasi ya kufuzu kwenda Gabon. Stars itaialika Misri kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam mwezi June kabla ya kusafiri kuifata Nigeria mwezi September kwenye mchezo wa mwisho.
Timu ya taifa ya Rwanda ‘The Amavubi’ imejiweka pazuri kwenye mbio za kuwania kufuzu kucheza fainali za AFCON mwaka 2017 huko Gabon baada ya kuibuka na ushindi mnono wa bao 5-0 dhidi ya Mauritius kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Amahoro, Kigali, Rwanda.
Ernest Sugira alifunga mabao mawili ya haraka kabla ya Dominique Nshuti  kupachika bao la tatu lililoifanya  Rwanda kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 3-0.
Baada ya mapumziko Fitina Omborenga na Jean-Baptiste Mugiraneza walifuta machungu ya kichapo cha 1-0 walichopata katika mechi ya ugenini siku tatu tu zilizopita kwa kufunga magoli mengine mawili na kukamilisha ushindi wao wa magoli 5-0.
Kufuatia ushindi huo Rwanda imeimarika hadi nafasi ya pili katika kundi lake wakiwa na alama 6, nne nyuma ya Black Stars ya Ghana.
Katika matokeo mengine, Ethiopia ilikomaa na kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Desert Foxes ya Algeria mjini Addis Ababa.
Algeria ambao wanaongoza kundi lao walilazimika kufanya kazi ya ziada baada ya wenyeji wao kuongoza mara mbili.
Algeria waliichapa Ethiopia 7-1 mjini Blida timu hizo zilipokutana Ijumaa iliyopita katika mechi ya kwanza.
Licha ya matokeo hayo, Algeria wanaongoza kundi J wakiwa na alama 10, alama 5 zaidi ya Ethiopia.
Uganda wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wameshindwa kutamba mbele ya Burkina Faso na kujikuta ikilazimishwa sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa marudiano baada ya kuchapwa bao 1-0 ugenini kwenye mchezo wa kwanza .
Kila mshindi katika makundi yote 13 atajikatia tiketi ya moja kwa moja kucheza Gabon.
Hata hivyo timu mbili zilizomaliza na alama nyingi katika nafasi ya pili pia zitajiunga na mwenyeji katika kindumbwendumbwe hicho.
Huu hapa mukhtasari wa matokeo ya mechi zilizochezwa Jumanne.
Rwanda 5-0 Mauritius
Namibia 1- 3 Burundi
Malawi 1-2 Guinea
Togo 0-0 Tunisia
Angola 0-2 DR Congo
Liberia 5-0 Djibouti
Uganda 0-0 Burkina Faso
Ethiopia 3-3 Algeria
Niger 1-2 Senegal
Namibia 1-3 Burundi
Togo 0-0 Tunisia
Sudan 1-1 Ivory Coast
Misri 1-0 Nigeria
Lesotho 2-1 Seychelles
Malawi 1-2 Guinea
Gambia 0-0 Mauritania
Afrika Kusini 0-0 Cameroon
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni