Cristiano Ronaldo kwa mara nyingine alikuwa kwenye kiwango cha juu baada ya kuisaidia timu yake ya taifa kupata ushindi wa magoli 2-01 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ubelgiji uliopigwa Jumanne usiku.
Ndani ya dakika 10 za kwanza, Ronaldo alifanya shambulio la hatari lililomuacha hoi beki wa Ubelgiji Jason Denayer.
Ronaldo alitengeneza nafasi mbili za kupachika bao laikini timu yake ilishindwa kufanya hivyo kutokana na uimara wa golikipa wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Thibaut Courtois.
Hatimaye Ureno ilipata bao dakika ya 20 lililofungwa na Nani kabla ya Cristiano Ronaldo kupachika bao la pili dakika tano kabla ya kwenda mapumziko.
The Real Madrid superstar headed home from a João Mário cross and celebrated in typical style.
Superstar huyo wa Real Madrid alifunga bao lake kwa kichwa akiunganisha krosi ya João Mário kisha kushangilia kwa style ya aina yake. Hilo ni bao la 47 kwa Cristiano Ronaldo msimu huu.
Romelu Lukaku aliifungia Ubelgiji goli la kufutia machozi akiunganisha kwa kichwa krosi ya mdogoake Jordan Lukaku.
0 maoni:
Chapisha Maoni