Mambo bado yameendelea kumwendea poa Vardy msimu huu, baada ya kuiongoza Leicester kukaa kileleni mwa Premier League, ameifungia England magoli mawili ndani ya siku nne.
Kipindi cha kwanza hakikikuwa kizuri kwa England dhidi ya Uholanzi iliyoonekana kujichokea, lakini kabla ya mapumziko Jamie Vardy aliipa goli England kutokana na shambulio zuri lililofanywa na Three Lions.
Goli la England lilianza kutengezwa na Adam Lalana kisha Kyle Walker akahusika kwenye mapishi ya goli hilo ambapo kama kawaida yake Vardy hakufanya makosa akaupeleka mpira kambani na kuandikia imu yake bao la kuongoza dakika ya 41 ya mchezo.
Vincent Janssen aliisawazishia Uholanzi kwa mkwaju wa penati dakika ya 50 kipindi cha pili baada ya beki wa England Danny Rose kuunawa mpira kwenye box kufatia mashambulizi ya kila mara yaliyofanywa na Uholanzi langoni mwa ‘Simba watatu’ na kusababisha presha kuwa kubwa.
Luciano Narsingh aliifungia Uholanzi bao la ushindi akiunganisha krosi ya Phil Jagielka zikiwa zimesalia dakika 13 mchezo kumalizika.
Takwimu unazotakiwa kuzifahamu:
- Vardy ameifungia England bao la 100 ikiwa chini ya Hodgson.
- Goli lililofungwa na Janssen lilikuwa ni goli la kwanza England kufungwa ndani ya dakika 443 kwenye uwanja wa Wembley.
- Ilikuwa ni mara ya kwanza England kuruhusu magoli mawili kwenye uwanja wa Wembley tangu November 2013 dhidi ya Chile.
- England haijashinda dhidi ya Uholanzi kwenye m,ichezo saba ya mwisho waliyokutana (D4 L3).
0 maoni:
Chapisha Maoni