Wazungu mara nyingi ni watu ambao wanaheshimu rekodi katika maisha yao ya kila siku, toka aondoke Alex Ferguson Man United kuna makocha wawili sasa wameingia kuifundisha Man United.
David Moyes ndio kocha wa kwanza kuingia Man United baada ya kuondoka kwa Alex Ferguson aliyedumu na klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 20, Moyes aliingia 2013 na kutimuliwa 2014 lakini David Moyes ameondoka Man United akiwa kaharibu rekodi zaidi ya 8 katika kipindi kifupi.
Baada ya Moyes akaingia Louis van Gaal ambaye nae usiku wa March 17 ameharibu rekodi ya Man United iliyodumu kwa miaka 60 baada ya kutolewa na Liverpool katika michuano ya Europa Ligi kwa jumla ya goli 3-1. Liverpool ndio imekuwa klabu ya kwanza kuitoa Man United katika michuano ya Ulaya baada ya miaka 60 kupita.
0 maoni:
Chapisha Maoni