Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona yaHispania Lionel Messi ameweka na kuvunja rekodi nyingi akiwa ndani ya klabu ya FC Barcelona ya Hispania, ila March 15 101greatgoals.com ndio wametaja rekodi inayomsumbua Lionel Messi kwa sasa.
Lionel Messi kwa sasa anatajwa kuwa na wakati mgumu wa kuivunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Ronald Koeman ambaye anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi kwa faulo, Koeman kafunga jumla ya faulo 25 kuanzia mwaka 1989-1995.
Lakini Lionel Messi kafunga jumla ya faulo 21 kuanzia 2004 hadi sasa, huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Ronaldinho ambaye kafunga faulo 20 kuanzia mwaka 2003-2008. Hiyo ndio rekodi pekee Lionel Messi rekodi hajaivunja hadi sasa.
0 maoni:
Chapisha Maoni