Klabu ya Dar Es Salaam Young Africans Jumamosi ya March 19 itarudiana na klabu yaAPR ya Rwanda katika mchezo wake wa pili wa raundi ya pili ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Yanga itarudiana na APR baada ya mchezo wao wa kwanza waliocheza katika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda kuibuka na ushindi wa magoli 2-1, hivyo inahitaji hata sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele. Kuelekea mchezo huo kocha wa Yanga Hans van der Pluijm ameongea haya.
“Kwanza Juma Abdul hatocheza ana kadi mbili za njano, pili baadhi ya wachezaji wetu wawili Matheo na Said wanasumbuliwa na Malaria tunatarajia watapona na kurejea kikosini mapema, lakini kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi tunashambulia pale inapohitajika na kujilinda pale inapohitajika” >>> Hans van der Pluijm
0 maoni:
Chapisha Maoni