Matumaini ya Manchester City ya kutaka kushinda ligi ya Uingereza msimu huu yamedidimia baada ya kutoka sare ya 0-0 na kilabu ya Norwich City na hivyobasi kusalia nyuma ya viongozi wa ligi Leicester kwa pointi tisa zikiwa zimesalia mechi tisa.
Kipa wa Norwich alilazimika kufanya kazi ya ziada ili kuzuia mashambulio mawili ya Sergio Aguero huku timu hiyo ya nyumbani ikifanikiwa kuizuia miamba ya City.
Hatahivyo,ilikuwa Norwich ambayo karibia ifunge bao baada ya shambulio la Patrick Bamford kugonga mwamba wa goli.
Norwich ingejiweka kifua mbele lakini shambulizi la Graham Dorrans ililotoka nje.
0 maoni:
Chapisha Maoni