KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Van Der
Pluijm ameipongeza timu yake baada ya ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya APR
katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika uliochezwa juzi kwenye
Uwanja wa Taifa wa Amahoro Kigali, Rwanda.
Magoli ya Yanga yalifungwa na Juma
Abdul katika dakika ya 20 na Thaban Kamusoko katika dakika ya 72, huku
goli la kufutia machozi la APR likiwekwa kimiani na Patrick Sibomana
katika dakika ya 92 ya mchezo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka
Rwanda, Pluijm amefurahishwa sana na vijana wake kuweza kuondoka na
ushindi huo wa mabao 2-1 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga
mbele.
“Nimefurahi sana ila napenda kuwaambia
wachezaji wangu lazima tuwe makini kuelekea mchezo wetu wa marudiano kwa
sababu tumejua jinsi gani wapinzani wetu wanacheza na kwangu naona
itakuwa mechi ngumu sana,” alisema.
Pluijm alisema hangependa kuongelea
sana kuhusu wapinzani wake, lakini anachotaka kusema wapinzani wake
wameonesha mchezo mzuri na sio timu ya kuibeza. “Mpira ni mchezo wa
makosa wenzetu walifanya makosa na sisi tumeweza kuyatumia yale makosa
waliofanya,” alisema.
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa APR,
Mtunisia Nizar Khanfir alisema wamepoteza mchezo kutokana na makosa
waliofanya na waliweza kuadhibiwa kwa kufungwa 2-1. “Mechi bado ipo wazi
inatakiwa tufanye bidii tushinde mechi yetu ya pili Jumamosi ijayo
nchini Tanzania. Makosa tuliyofanya yanaweza kuepukika,ila nina imani
kuwa tunaweza kufanya vizuri katika mechi yetu inayokuja,”alisema
Kanifir.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Chapisha Maoni