AZAM YATUPWA NJE MICHUANO YA AFRIKA

Farid Musa
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azan FC wametupwa nje ya michuano ya hiyo baada ya kuchapwa kwa magoli 3-0 na Esperance ya Tunisia kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Tunis, Tunisia.
Azam walikomaa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kwenda mapumziko wakiwa hawajaruhusu goli hata moja licha ya mashambulizi makali ya mara kwa mara kufanywa kwenye goli lao lakini golikipa Aishi Manula alikuwa imara kuondosha hatari zote na kuiweka Azam salama.
Dakika ya 49 kipindi cha pili Esperance walipata bao la kuongoza lililopachikwa kambani na Saad Bguir kisha Jouini akaiandika bao la pili na Ben Yousef akaihakikishia timu yake kusonga mbele baada ya kufunga bao la ushindi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika.
Benchi la ufundi la Azam chini ya Stewart Hall lilifanya mabadiliko kujaribu kubadili matokeo kwa kuwapumzisha Farid Musa, Salum Abubakar ‘Sure Boy’na Wazir Salum huku nafasi zao zikichukuliwa na Hamisi Mcha, Himid Mao na Didier Kavumbagu lakini bado mabadiliko hayo hayakumlipa kocha huyo raia wa England.
Esperance imeitupa Azam nje ya mashindano kwa jumla ya magoli 4-2 baada ya kucheza mechi mbili. Mchezo wa kwanza Azam ikiwa nyumbani ilishinda kwa magoli 2-1 lakini leo imejikuta ikikubali kuchapwa magoli 3-0 ndani ya dakika 32 na kuyaaga mashindano rasmi.
Wachezaji wa kikosi cha Azam wakihamasishana kabla ya kuanza kwa mechi yao dhidi ya Esperance
Wachezaji wa kikosi cha Azam wakihamasishana kabla ya kuanza kwa mechi yao dhidi ya Esperance
Himid Mao (kulia) lakini aliingia badaye dakika ya 79, Mao pia hakucheza kabisa kwenye mchezo wa awali uliozikutanisha klabu hizo jijini Dar es Salaam
Himid Mao (kulia) lakini aliingia badaye dakika ya 79, Mao pia hakucheza kabisa kwenye mchezo wa awali uliozikutanisha klabu hizo jijini Dar es Salaam
Mashabiki wa Esperance
Mashabiki wa Esperance wakiendelea kuingia kwa wingi uwanjani kui-support timu yao kwenye uwanja wao wa nyumbani ilipokuwa ikikabiliana na Azam FC 
Azam-Tunis 2
Juma lililopita kuna taarifa zilitoka zikisema Farid Musa amesafiri kuelekea Hispania kufanya majaribio kwenye klabu moja ya kuko, lakini alionekana kwenye kikosi cha Azam kilichocheza dhidi ya Esperance na kuzua maswali mengi kwa watu

Farid Musa akitolewa nje ya uwanja kwa gari maalum la kubebea wagonjwa wanaoumia uwanjani
Farid Musa akitolewa nje ya uwanja kwa gari maalum la kubebea wagonjwa wanaoumia uwanjani kama kwenye baadhi ya viwanja vya Ulaya
Sure Boy (kushoto) alianza kwenye mchezo wa jana licha ya kuwepo taarifa kwamba kulikuwa na mashaka ya kumkosa, hata hivyo alipumzishwa dakika ya 79 kipindi cha pili
Sure Boy (kushoto) alianza kwenye mchezo wa jana licha ya kuwepo taarifa kwamba kulikuwa na mashaka ya kumkosa, hata hivyo alipumzishwa dakika ya 79 kipindi cha pili
Allan Wanga (wa kwanza kushoto) na wachezaji wengine wa Azam wakiwa benchi, mchezaji huyo wa Kenya amekuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Azam kutokana na kukosa kabisa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Azam

Ramadhani Singano (Messi) amekuwa ni msaada mkubwa kwenye kikosi cha Azam siku za usoni tangu aliojihakikishia nafasi kwenye kikosi hicho. Messi ndiye aliyefunga goli la pili dhidi ya Esperance kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Dar

Azam-Tunis 9

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni