Chelsea imetangaza rasmi kwamba Antonio Conte ni kocha mpya wa klabu hiyo atakaeanza kuliongoza benchi la ufundi la The Blues mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro huko nchini Ufaransa.
Tarifa zilishavuja kitambo kidogo kwamba Conte atachukua kibarua cha kuinoa Chelsea japo ilikuwa inatarajiwa mambo yangewekwa hadharani baada ya kumalizika kwa michuano ya mataifa ya Ulaya wakati wa majira ya joto.
Leo April 4, klabu ya Chelsea imethibitisha kukubaliana Conte kuwa kocha wao akichukua mikoba ya aluyekuwa kocha wa timu hiyo Jose Mourinho.
Conte amesaini deal la miaka mitatu na The Blues, kisha akatoa maneno yafuatayo kwenye website ya Chelsea:
Nimefurahi sana kupata fursa ya kufanya kazi kwenye klabu ya Chelsea. Najivunia kuwa kocha wa timu ya taifa ya nchi yangu pia kuivutia klabu kama Chelsea na kupewa jukumu la kuifundisha.
Natarajia kukutana na kila mmoja kwenye klabu pamoja na kupambana kila siku na changamoto za michuano ya Premier League.
Chelsea pamoja na soka la Engand linatazamwa popote utakapoenda, lengo langu ni kupata mafanikio zaidi kama yale ambayo nimekuwa nikiyafurahia Italy.
Nimefurahi tumeshaweka wazi kilakitu kwahiyo kilakitu kiko sawa na tumemaliza tetesi zote. Nitaendelea na kazi yangu kama kocha wa timu ya taifa ya Italy na kwasasa sitazungumza tena kuhusu Chelsea hadi fainali za Euro zitakapomalizika.
Inaripotiwa Conte alimtupa mpinzani wake kocha wa Chile Jorge Sampaoli kwenye kinyang’anyiro hicho na amekuwa kwenye mazungumzo na mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich kwa miezi kadhaa iliyopita.
0 maoni:
Chapisha Maoni