Wolfsburg imeishangaza Real Madrd baada ya kuicharaza kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ikiwa ni hatua ya robo fainali.
Wenyeji hao walipewa penati iliyozua utata kufatia Casemiro kudaiwa kumfanyia madhambi Andre Schurrle penati ambayo ilisukumwa kambani na Ricardo Rodriguez.
Safu ya ulinzi ya Real Madrid ilikuwa dhaifu ilishuhudiwa ikimruhusu Bruno Henrique kutengeneza bao la pili lililofungwa na Max Arnold.
Madrid walijitahidi kupambana kubadili matokeo ya mchezo lakini haikuwa rahisi kufanya hivyo huku wakiwa wamebaniwa penati ya mapema.
Kichapo hicho kimekuwa ni cha kwanza kwa Real Madrid kwenye robo fainali ya Champions League tangu mwaka 2004 na kinawapa kibarua cha ziada kwenye mchezo wao wa marudiano Jumanne ijayo kwenye uwanja wa Bernabeu.
Rekodi muhimu unazopaswa kuzifahamu
- Navas amefungwa kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Champions League baada ya kucheza kwa dakika 738 bila nyavu zake kutikiswa.
- Real wamefungwa magoli 2-0 kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya tangu mwaka 2014 ambapo walichezea kichapo kutoka kwa Borussia Dortmund. Hiyo ilikuwa mara yao ya mwisho kupoteza mchezo kwa magoli mawili.
- Wolfsburg sasa wanafanikiwa kushinda mchezo wa tano wa Champions League mfululizo.
- Wamepoteza mechi moja kati ya mechi zao nane za nyumbani za Champions League, walifungwa na Manchester United kwa magoli 3-1 December 2009.
0 maoni:
Chapisha Maoni