La Liga: Barca watahitaji kuiondoa ‘laana’ ya Uwanja wa Anoeta ili kuifunga Sociedad kesho

FC Barcelona Jumamosi ya kesho watasafiri kutoka kwao kwenda mpaka kwenye uwanja ambao wamekuwa wakipata matokeo yasiyoridhisha katika miaka ya hivi karibuni. 
  Katika mechi 5 zilizopita ambazo Barca alicheza kwenye uwanja huo hajafanikiwa kushinda hata mchezo mmoja. Sio Pep Guardiola, Sio Tito Vilanova, wala Tata Martino ambaye alipata ushindi katika uwanja huo – na Luis Enrique alipoteza mechi uwanjani hapo msimu uliopita. 
Makocha wanne wa Barcelona wote waliangushwa na ‘laana’ ya uwanja wa Anorta unaotumiwa na klabu ya Real Sociedad. Barca wamefanikiwa kupata pointi kati ya 15 tangu Sociedad walipopanda daraja. Barcelona walipata sare ya 1-1 katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya Copa Del Rey msimu wa  2013-14.  
Inaonekana ni jambo la kimiujuza ukiangalia na mafaniko makubwa waliyoyapata FC Barcelona katika miaka ya hivi karibuni. Makombe matatu ya ligi, Copa Del Rey mawili, Matatu ya Spanish Super Cups, mawili ya Champions League, mawili ya kombe la dunia kwa vilabu na matatu ya  European Super Cups.
  
FC Barcelona wamefungwa mechi kati ya tano walizocheza katika uwanja wa wa Anoeta, lakini kati ya hizo 4, mechi 3 Real Sociedad walitoka nyuma na kuja kuwafunga wakatalunya. Katika mechi waliyotoka sare Barcelona walikuwa mbele kwa 2-0 baada ya dakika 10 tu za mchezo.  
  
  Mfululizo wa matokeo ya kutokuridhisha yalianza msimu wa 2010-11. Thiago alifunga goli dakika ya 28, lakini Ifran akasawazisha dakika ya 70 na  Xabi Prieto (80) akafunga la ushindi. Msimu uliofuatia Xavi akafunga goli dakika (9) na Cesc Fabregas (10) akaongeza la pili, lakini Agirretxe (58) na Griezmann (60) wakasawazisha. 
Msimu wa 2012-13, Tito Vilanova alipata kipigo chake cha kwanza cha ligi. Barcelona walianza kufunga kwa magoli ya Messi dakika ya na Pedro (24) lakini Real wakarudisha kupitia Chory Castro (40), Mascherano akajifunga dakika ya (62) na Agirretxe akafunga la ushindi dakika (87).
Tata Martino pia nae yalimkuta,  Alex Song alijifunga dakika (31). Messi akasawazisha (35) lakini Griezmann (53) na Zurutuza (58) wakawanyoosha Barcelona.
Msimu uliofuatia Jordi Alba alijifunga dakika ya 2, na goli hilo likatosha kumpa Enrique kionjo cha kichapo kutoka kwa Sociedad. 
Unapofananisha matokeo haya ya Barca katika uwanja huu na viwanja vingine ambavyo La Blaugrana hupata taabu – utaona kwamba ‘laana’ ya Anoeta Stadium ilivyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni