Tayari ratiba ya nusu fainali ya michuano ya UEFA Champions League imeshatoka baada ya kuchezeshwa draw ya kutafuta nani ataumana na nani kati ya vilabu vinne vilivyosalia kwenye michuano hiyo baada ya Jumanne na Jumatano kushuhudia vilabu vingine vinne vikiyaaga mashindano hayo ikiwa ni pamoja na bingwa mtetezi Barcelona.
Manuel Pellegrini atarejea kwenye klabu yake ya zamani baada ya Manchester City kujikuta ikitakiwa kupambana na miamba ya Hispania Real Madrid wakati Atletico Madrid watakwaana na kikosi cha Pep Guardiola Bayern Munich mechi ambazo zitapigwa April 26/27 na May 3/4.
Atletico Madrid v Bayern unatarajiwa kuwa mchezo wa ina yake uliojaa mbinu na ufundi mwingi kutokana na makocha wa timu hizo kufahamiana vizuri kwasababu walishawahi kuchuana kwenye ligi ya Hispania La Liga wakati Pep akiwa kocha wa klabu ya Barcelona. Kunauwezekano wa kuwepo fainali ya Madrid derby endapo vilabu vyote vya Hispania vitafuzu hatua ya fainali kitu ambacho kilitokea mwaka 2014.
Kitu kingine kizuri ni kwamba, endapo The Bavarians na Manchester City zitafuzu hatua ya fainali, Pep Guardiola atakutana na timu yake atakayoifundisha msimu ujao.
Ratiba kamili ya hatua ya nusu fainali klabu bingwa Ulaya ipo kama ifuatavyo;
0 maoni:
Chapisha Maoni