ROONEY AELEZA CRUYFF ALIVYOMZUIA KUTWAA CHAMPIONS LEAGUE MARA MBILI
-Striker wa Manchester United Wayne Rooney ameonesha heshima kwa nguli wa soka Johan Cruyff kwa kusema kwamba, kama isingekuwa kazi yake ya kutukuka kwenye klabu ya Barcelona, angekuwa ameshinda medali mbili zaidi za ligi ya mabingwa Ulaya.
Nyota huyo raia wa Uholanzi alifariki dunia wiki iliyopita baada ya kupambana na kansa ya pafu, aliifundisha Barcelona kwa miaka nane na kuanzisha style ya mchezo inayoindwa tik-tak mwanzoni mwa miaka ya 1990 iliyowafanya miamba hao wa soka la Hispania kuwa wafalme wa soka duniani tangu kipindi hicho hadi sasa.
Barcelona illichapa Manchester United kwenye fainali mbili za ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2009 (2-0) na 2011 (3-1) na Rooney alikuwepo mara zote kwenye kikosi kilichopoteza fainali zote mbili, lakini mafanikio ya klabu hiyo yamekuja kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Cruyff, alisema Rooney kuelekea mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya England dhidi ya Uholanzi ambapo England ilichapwa magoli 2-1.
“Unaona Barcelona namna inavyocheza leo na mafanikio waliyonayo, yote yanatokana na Cruyff”, alisema Rooney.
“Kama asingekuwa yeye, huenda ningekuwa nimetwaa medali mbili nyingine za Champions League.”
0 maoni:
Chapisha Maoni