Ferguson – “Guardiola hawezi kufikia level ya Barcelona ndani ya EPL”
-Msimu ujao kwenye EPL kutakua na moja ya kocha bora kwenye ligi za Ulaya naye ni Pep Guardiola akiiongoza club ya Manchester City.
Sir Alex Ferguson mwenye miaka 74 ameulizwa swali kuhusu ujio wa Pep ndani ya EPL. Majibu ya Pep yalikua kama hivi , “Bila kujiuliza maswali mengi Pep ana ethics nzuri kwenye kazi yake, anafanya hivyo kwenye muda wa mazoezi hadi muda wa mechi. Yeyote anayedhani kwamba Pep atashindwa kwenye EPL basi inabidi abadirishe mawazo. Man City wamefanya kitu kizuri kumchukua kwenye timu yao. Lakini Pep hata kutana na vitu virahisi kwenye EPL, kila kocha anayetoka nje ya England lazima atakwambia ugumu wa EPL. Pep anaweza kufanikiwa ndani ya EPL lakini sidhani kama atafikia level ya mafanikio kama alivyokua na Barcelona, ile ilikua level nzuri sana na walikua vizuri”
0 maoni:
Chapisha Maoni