Kutana na story 5 kubwa zinazotawala vyombo vya habari vya majuu leo zikihusisha klabu ya Chelsea kutenga dau la £64m kwa ajili ya kumnasa mchezaji anayewaniwa na Manchester United, star wa Manchester United anataka kujiunga na West Ham kipindi cha usajili wa dirisha kubwa, Liverpool tayari imeshanasa saini ya kocha wa zamani wa Bayern Munich na star wa Chelsea yuko tayari kujiunga na Real Madrid kwa dau la £32m.
Star wa Manchester United kutimkia West Ham wakati wa usajili wa majira ya joto
West Ham United wanaonekana kutaka kutumia faida ya Manchester United kutompa mkataba mpya Michael Carrick ili kuinasa saini na kiungo huyo mkongwe. Gazeti la The Sun limeripoti kwamba, wagonga nyundo hao wanataka kumrejesha mchezaji wao wa zamani wakati wa usajili wa majira ya joto.
Carrick is a graduate of the West Ham youth academy and played for the Hammers first team for five years before moving to Tottenham.
Carrick ni zao la timu ya vijana ya West Ham na alikitumikia kikosi cha kwanza kwa miaka mitano kabla ya kujiunga na Tottenham.
Nyota huyo mwenye miaka 34 yupo kwenye mwaka wake wa mwisho wa mkataba ndani ya Old Trafford na anatarajia kurejea kwenye klabu iliyomlea kama hawatakubaliana deal jipya na the Red Devils.
Chelsea imetenga kiasi cha £64m kumsaini nyota anayewaniwa na Manchester United
Chelsea inaipiga kumbo Manchester United kwenye mbio9 za kumuwania star wa Real Madrid Sergio Ramos baada ya kuweka offer mezani ya kiasi cha £64million, hii ni kwa mujibu wa ripoti za Don Balon.
Mlinzi huyo wa kati mwenye miaka 30 sasa, amekuwa kwenye mipango ya usajili wa United tangu dirisha la majira ya joto la msimu uliopita lakini mwisho wa siku vilabu hivyo viwili vilishindwa kutekeleza deal hilo.
Antonio Conte ambaye atajiunga na Chelsea kama kocha wa kudumu wakati wa majira ya joto barani Ulaya, inasemekana kocha huyo wa zamani wa Juventus anatarajia kumuongeza kikosini beki huyo tumaini la Real Madrid.
Liverpool imemsajili kocha wa fitness Andreas Kornmayer kutoka Bayern Munich
Liverpool imemnasana kocha wa Bayern Munich Andreas Kornmayer kwa ajili ya kutengeneza fitness ya wachezaji wake na wanatarajia kumtambulisha rasmi kikosini msimu ujao.
Jugen Klopp anatarajia kufanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi chake kwa kuongeza wataamu kadhaa kwa ajili ya kumsaidia baada ya kumalizika kwa majira ya kiangazi.
Kwa nujibu wa The Mirror, Kornmayer atachukua nafasi ya kocha wa fitness wa sasa Ryland Morgans na ataongeza uzoefu unaohitajika kwenye kikosi cha Liverpool akiwa ameshaitumikia he Bavarians kabia miaka 10.
Stars wa Chelsea amekubali dau la £32m kwa ajili ya kujiunga na Real Madrid
Eden Hazard amekubali dau la £32m kujiunga na Real Madrid kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Hispania. Wiger huyo amekuwa akipambana kurejea kwenye form yake msimu huu huku akiwa bado anatafuta kufunga goli lake la kwanza kwenye Premier League msimu huu.
Hata hivyo, Hazard bado anatazamwa na anahitajiwa na miamba ya Bernabeu. (OK Diario)
Antonio Conte kumsajili star kutoka Juventus
Boss mpya wa Chelsea Antonio Conte yuko katika mbio za kumnasa striker wa Juventus Alvaro Morata ili kuimarisha safu yake ya ushambulizi.
Muhispania huyo alitarajiwa kurejea Real Madrid majira ya kiangazi lakini tetesi zinadai kwamba, The Los Blancos wanajipanga kumuuza kwa dau nono. (Calcio Mercato)
0 maoni:
Chapisha Maoni