Timu anayoinoa Kocha Selemani Matola ya Geita Gold Mine imeteremshwa daraja hadi la pili.
Geita imepatikana katika hatia ya upangaji matokeo katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya JKT Kanembwa ambayo pia imeteremshwa daraja.
Katika mechi hiyo, Geita Gold Mine ilishinda kwa mabao 8-0 na JKT Oljoro ikakubali kipigo cha mabao 7-0 kutoka kwa Polisi Tabora, timu hizo mbili pia zimeteremshwa daraja pia kwa kuhusishwa na upangaji wa matokeo.
Ila JKT Kanembwa iliyokuwa imeteremka daraja yenye inashushwa hadi Ligi ya Mkoa.
Uamuzi huo wa kamati ya nidhamu ya TFF, umetangazwa leo mchana lakini uongozi wa Geita Gold Mine umesisitiza kwamba utakata rufaa kwa kuwa hakuna sehemu inayoonyesha timu yao ilipanga matokeo.
Uamuzi huo wa kamati ya nidhamu ya TFF, umetangazwa leo mchana lakini uongozi wa Geita Gold Mine umesisitiza kwamba utakata rufaa kwa kuwa hakuna sehemu inayoonyesha timu yao ilipanga matokeo.
0 maoni:
Chapisha Maoni